Top Stories

‘Serikali kuokoa Bilioni 33 kwa Mwaka’- Waziri Gwajima

on

NI Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ambapo leo amezungumza na kusema kuwa Serikali itaokoa Bilioni 33 kwa mwaka kwa ajili ya ununuzi wa Dawa na Vifaa tiba baada ya kukamilika kwa ujenzi wa viwanda vya dawa na Vifaa tiba kinachojengwa Mkoani Njombe.

Waziri huyo ameyasema hayo baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Idofi-Makambako mkoani hapo.

“Hapa nimeangalia takwimu zako Mkurugenzi tunapoenda kukamilisha kiwanda hiki Cha mipira ya mikono(gloves), Dawa za vidonge (tablet), vidonge vya rangi mbili (Capsules) na dawa za maji(Syrup) Serikali kwa mwaka inakwenda kuokoa Bilioni 33 ambazo zingehitajika kununua mahitaji hayo”.

Aliongeza kuwa Serikali ingehitaji Bilioni 33 zaidi ili kwenda kununua dawa na Vifaa hivyo sehemu nyingine ndani au nje ya nchi lakini hizo Bilioni zinazoenda kuokolewa tunakua tumeshazalisha kwa gharama za uzalishaji kwa mwaka Bilioni 15.

“Ina maana hii Bilioni 33 inayobaki ukigawanya kwa milioni 700 ambayo ndio gharama za Kujenga vituo vya afya na Vifaa vyake kwa ‘force account’ Ni sawa na kujenga vituo vya afya 43”.Alifafanua Dkt.Gwajima

Alisema Mradi huo unafanya kutimiza azma ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi na Ilani yake inayosimamiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa lengo la kuhakikisha tunakuwa na uwezekano wa kupunguza gharama za kununua bidhaa ambazo tunaweza kuzitengeneza badala ya kuzinunua nje zitanunuliwa hapa hapa.

 

Tupia Comments