Baada ya Waziri wa Madini, Dkt Dotto Biteko kuzindua kituo cha shughuli za utalii wa madini pamoja na uuzaji wa madini hatimaye kituo hicho kimetengeneza maporomoko ya maji nakuyapa jina la Rais wa Tanzania
Dkt Biteko wakati akizindua kituo hicho cha Tanzanite Experience kilichopo Kibaoni wilayani Karatu Mkoani Arusha amesisitiza Serikali kupitia Wizara hiyo kuendelea kushirikiana na wawekezaji wa sekta ya Madini Katika kuongeza thamani shughuli za Utalii wa Madini ya Tanzanite ikiwa ni zao jipya la Utalii nchini Tanzania kufutia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupigia chapuo madini hayo kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania.
Akiwa Mkoani Arusha eneo la Kibaoni nje kidogo ya Wilaya Karatu, katika uzinduzi wa kituo cha Tanzanite Experience ambacho ni maalumu kwa ajili ya shughuli za Utalii pamoja na uuzaji wa Madini ya Vito nchni.
Mkurugenzi wa kituo hicho Hasnain Sajan amesema lengo la kuweka maporomoko hayo ni kutambua kazi anayoifanya Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Kwa sasa kituo hicho kimeajiri zaidi ya watanzania 80, na uwekezaji wake u atajwa kufikia zaidi ya bilioni 1.4 za kitanzania.