Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt . Dotto Biteko amesema serikali itaongeza upatikanaji wa gesi ili kufidia mapungufu ya umeme nchini kutokana na upungufu wa maji katika mabwawa yanayozalisha umeme
Dkt Biteko amesema hayo wakati alipotembelewa bwawa la kuzalisha la umeme la Mtera lililopo mkoani Iringa na licha kujionea upungufu wa maji Katika bwawa hilo linalosababishwa na ukame kutokana na kuchelewa kwa mvua biteko amesema serikali itahakikisha inapambana kwa kila namna ili kuondokana na adha hiyo ya upungufu wa umeme nchini.
Dkt Biteko alisema serikali kwa kushirikiana na TANESCO itahakikisha kila linalowezekana ili kuzidi kubuni vyanzo vya upatikanaji umeme ikiwemo gesi ili kuhakikisha umeme unapatikana ili shughuli za kiuchumi kwa watu zisiathirike kutokana na umeme
“ Kazi yetu sisi kama serikali ni kuhakikisha tunawaondolea wananchi Adha hii ya umeme kwa kutumia vyanzo vyingine vya kuzalisha umeme “
Vile vile Biteko amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji kwa sababu uchumi wa wananchi wa Tanzania unategemea sana upatikanaji wa umeme hivyo shughuli zote za kimazingira zikiathiriwa, zinaathiri pia upatikanaji wa umeme