SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema itaendelea kuwekeza katika matumizi ya Tehama ili wanafunzi waweze kupata ujuzi na maarifa yatakayowasaidia katika maisha yao ya baadae.
Ofisa kutoka Wizara ya Elimu kitengo cha TEHAMA Sadik Makanyaga katika hafla ya ufunguzi wa chumba cha maabara ya TEHAMA chenye kompyuta 20 katika skuli ya Sekondari Mkwajuni kilichofadhikiwa na kampuni Helios Towers.
Alisema matumizi ya Tehama yana umuhimu mkubwa katika kuwajenga vijana kitaaluma zaidi kwani hivi sasa dunia imeshapiga hatua katika matumizi hayo.
Aidha alisema walimu wafahamu sasa wanaondoka katika matumizi ya makarstasi na chaki kwani hivi sasa watu wanakwenda kiteknolojia.
Hivyo alisema ni matarajio yake kwamba vifaa hivyo vinatumika ipasavyo katika kuwafundisha watoto kiteknologia kufundisha kupitia mtandao kwani huko nchi nyingi ndipo zilipo.
Afisa huyo aliwaasa wanafunzi kuacha kudharau matumizi ya TEHAMA katika Elimu ambayo yatawasaidia kupata maendeleo makubwa pale watakapomaliza masomo kuweza kujiajiri na kuajiriwa.
“Wanafunzi mmepatiwa nyinyi kompyuta hivi lengo la wafadhili ni kuwasaidia nyinyi kuingia katika Tehama badala yake kunitumia fursa ili kufahamu mbinu na kuweza kufanya vizuri katika mitihani kwa kutumia tehama.
Aliiitaka kamati ya skuli kuhakikisha wanasimamia vifaa hivyo kupitia walimu ili kuona vinadumu kwa muda mrefu na kuona zinadumu kwa wanafunzi wa sasa na wanaokuja.
Alisema idara ya TEHAMA Itaendelea kuwapatia Mafunzo na kuyaendeleza Yale waliopewa na Camara Education Tanzania
Akizungumzia suala la internet alisema serikali ipo katika mpango wa kuzipatia internet skuli zote za Unguja na Pemba zinapata mabadiliko ya TEHAMA
Aliwapongeza wadau hao kwa kuwapatia kompyuta hizo kwani bado sekta ya Elimu bado inahitaji masuala ya Tehama hivyo wasisite kuendelea kuwasaidia ili watoto waende katika ulimwengu huo wa Tehama.
Naye alisema lengo la kufadhili maabara hiyo ya TEHAMA ni kuona wanafunzi wanaendelea kidigitali.
Mkurugenzi wa Helios Tower,Bwana Tom alisema, lengo ni kupata mawasiliano kuzunguka dunia yote hivyo aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidiii na kujiwekea ndoto zao za baadae ili nchi iweze kupata watalaamu katika nyanja mbalimbali ikiwemo mahandisi.