Serikali mkoani Morogoro imejipanga kuhakikisha inadhibiti mfumo wa wakulima wa zao la mpunga kuuza lumbesa za mpunga kwa kuweka mashine za kukoboa mpunga kila wilaya kupitia vyama vya ushirika ili waweze kuuza mchele nasi mpunga hatua inayolenga kuwaepusha na hasara wanazozipata kwa kuuza kwa bei ya hasara.
Mpango huo umeelezwa na mkuu wa mkoa wa Mrogoro Fatma Mwassa katika jukwaa la tatu la vyama vya ushirika mkoa wa Morogoro ambapo amesema wakulima wamekuwa wakiuza mpunga kwa bei ya hasara ikilinganishwa na gharama walizotumia hivyo serikali itaanzisha mashine za kukoboa mpunga ili wakulima wauze mchele utakao waletea faida zaidi.
Kwa upande wake mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Morogoro bwana Keneth Shemdoe ameeleza hali ya ushirika kwa mkoa wa Morogoro ambapo amesema kwasasa hali ya uzalishaji wa mazao imeendelea kuongezeka licha ya kuwa na changamoto za uhaba wa maafisa ushirika ambapo kwa mkoa wa Morogoro inajumla ya maafisa 20 peke.
Aidha mwenyekiti wa jukwaa hilo Idd Bilali amesema kwasasa bado wakulima wanakabiliwa na changamoto ya kuwa na masoko ya uhakika hali inayochangia wakulima kuuza mazao kwa bei ya hasara.