Mbunge wa Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haihusiki na jaribio la kuondoa maisha yake baada ya gari lake kushambuliwa kwa risasi.
Ole Sendeka amesema hayo katika Mji mdogo wa Orkesumet kwa mara ya kwanza baada ya kutokea tukio hilo “Bunduki mbili za kijeshi ambazo tumeokota maganda 15 ya risasi za bunduki za kijeshi na risasi 4 zimeingia katika gari langu mbili usoni moja ubavuni , kunusurika huko ni kwa neema ya Mungu”
“Serikali ya awamu ya sita haijahusika, CCM Oyeee, hivi ngoja niwaambieni hivi Mimi ningepigwa na Serikali ya CCM, Mimi ni Kichaa wa kuja kusema CCM oyee!? yaani Mimi nipigwe na Serikali ya CCM wanataka kuondoa uhai wangu niwaache Watoto wangu wadogo halafu Mimi ni Kichaa namuogopa nani!? nije niseme CCM Oyee, ni kwasababu nina uhakika kwamba Rais Samia na Uongozi wa Serikali ya CCM hawana mchango katika jaribio la kuondoa maisha yangu, wangehusika ningemtaja kwa jina mmoja hata Samia ningemtaja hata Rais ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu ningemtaja kwa jina hadharani”