Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiongozwa na Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha Sekta ya Elimu ya Juu kwa kuwezesha miundo mbinu ya kisasa kupitia mradi wa Elimu ya Juu na Mageuzi ya Kiuchumi.
Akizungumza katika halfa ya utiaji Saini ya mikataba hiyo makamu Mkuu wa Chuo Prof.Aloys Mvuma amesema kupitia Mradi huo utawesha chuo Cha Must kuchukua wanafunzi wengi zaidi lengo ni kufikia wanafunzi 15000 mwaka 2025. Majengo yanayotegemewa kujengwa ni Jengo la taaluma, kenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3200, Jengo la pili ni la ubunifu, na Jengo la tatu ni Jengo karakana na maabara.
Ujenzi huo unategemea kukamilika ndani ya miezi 18 kuanzia sasa.Mkandarasi wa mradi huo Mr.Peng Chai ameahidi kutekeleza mradi kwa wakati na Kwa ubora uliokusudiwa.