Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema hadi sasa hakuna Mtanzania aliyepata madhara yoyote kufuatia vita inayoendelea Ukraine na kusababisha Serikali ya Nchi hiyo kutangaza hali ya hatari.
Serikali imewaomba Watanzania wote wanaoishi Ukraine wakiwemo Wanafunzi, Wafanyabiashara na Wafanyakazi kuendelea kuwa Watulivu katika kipindi hiki ambacho Serikali inaendelea kufuatilia usalama wao kwa kushirikiana na Mamlaka mbalimbali za Ukraine.
MAPYA UKRAINE: RAIS AAGIZA WANAUME KUBAKI ILI KUILINDA NCHI KUTOKANA NA UVAMIZI WA URUSI