Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imepokea taarifa ya hali ya upatikanaji wa rasilimali fedha na utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Maji kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba 2024 na mwenendo wa ulipaji wa madeni ya wakandarasi wa ndani kwa mwaka 2024/2025
Taarifa hiyo imewasilishwa leo 21 January 2025, na Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) akiwa ameongozana na Menejiment ya
Wizara ya Maji katika kikao cha kamati hiyo jijini Dodoma.
Katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2024
Ambapo jumla ya Shilingi 241,981,968,116.05 zimetumika kulipa madai na madeni ya Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji nchini