Serikali, imeipongeza Sekta Binafsi, kwa mchango wake wa kuitimiza azma ya uzalishshaji wa ajira mpya , milioni 8 kufikia mwaka 2025 na kuahidi itazifanyia mapitio sheria zote za biashara ili kuboresha zaidi mazingira ya kufanya biashara nchini na kuiwezesha sekta binafsi kuzalisha ajira zaidi na zaidi na kuchangia kukua kwa uchumi na kuongeza pato la taifa.
Ahadi hiyo imetolewa na jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dr. Ashatu Kijaji, katika hafla ya kuwakabidhi zawadi za fedha taslimu Shilingi milioni 100, kwa washindi watatu wa kwanza wa shindano la ubunifu wa miradi kwa vijana wa Kitanzania, iliyofanyika jana usiku katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijjini Dar es Salaam.
Katika Hotuba ilityosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Ali Gugu, Waziri Kijaji amesema, sekta binafsi ndio injini ya uchumi wa taifa, hivyo serikali ya awamu ya 6, serikali imeahidi itaendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara ili wajasiriamali wadogo na wakati, wakuwe na kuzalisha kada ya mamilionea na mabilionea wa Kitanzania ambao watachangia katika ukuaji wa uchumi wa taifa.
Ali Gugu, ameipongeza Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies kwa shindano hilo, na kutoa zawadi za zaidi ya shilingi milioni 100, kati ya hizo, washindi watatu wa mwanzo, kila mmoja amepewa hundi ya shilingi 20 za Kitanzania kuboresha mitaji yao na kuwalea kwa mwaka mmoja kwa kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo, na kuwaangazia fursa za masoko.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TotalEnergies Tanzania, Jean-Francois Schoepp, mesema lengo la kampuni ya TotalEnergies, isio tuu kufanya biashara na kuzalisha faida, bali kuitumia hiyo faida inayopatikana na kuwajengea uwezo na wengine ili kuwainua Watanzania na kuliinua taifa kiuchumi.
Mkurugenzi Mkuu wa TotalEnergies Tanzania,Jean-Francois Schoepp, na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano, Getrude Mpangile, wanaeleza zaidi.
Shindano hilo la “STARTUPPER OF THE YEAR CHALLENGE BY TOTALENERGIES limefanyika katika nchi zaidi ya 50 barani Afrika, kwa Tanzania, wamejitokeza wajasiriamali zaidi ya 1000 kushiriki shindano hilo