Serikali imejibu kuhusu azimio la bunge la Umoja wa Ulaya kutaka uchunguzi huru ufanyike kuhusukumaliza sitofahamu kati ya Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro na Loliondo mkoani Arusha na mamlaka za hifadhi kwa kuzingatia misingi ya Haki za binadamu.
Azimio hilo limetolewa tarehe 14 Disemba baada ya kuwepo mjadala kuhusu haki za wananchi waliotajwa kwa jamii ya Masai wanaokaa karibu na hifaddhi ya Ngorongoro ambapo bunge hilo limeiomba Serikali ya Tanzania kuruhusu waangalizi wa Umoja wa Ulaya EU kutambelea katika maeneo yenye mgogoro.
Akijibu hoja hiyo mkurugenzi wa Habari Maelezo na Msemaji mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi amesema Serikali haitumii nguvu kuwaondoa wananchi wanaoishi katika maeneo ya Hifadhi ya Ngorongoro na kutaja kuwa zoezi hilo ni hiari na linazingatia haki za binadamu.
“Kilichotokea mwaka jana mwezi Mei kulikuwa na kundi la wananchi walisema wametoka Ngorongoro na walikwenda kutoa hoja zao na serikali ilipata nafasi ya kujieleza na mwezi wa nane mwishoni baadhi ya wabunge wa Bunge la Ulaya walitaka waje mwazoni mwa septemba ilikuwa ni muda mchache sana na Serikali iliwambia karibuni lakini mmetoa ombi lenu kwa siku chache sana tunaomba mjipange na sisi tujipange kuwapokea ili muelewe kinachozungumza”
Mobhare Matinyi Akizungumza kuhusu ushirika wa Tanzania na umoja wa Ulaya amesema Tanzania ni mshirika wa kimkakati wa umoja wa ulaya na kuwa “Serikali inauhusuano mzuri na umoja wa Ulaya na Kamishna wa Umoja wa Ulaya hivi karibuni amesema ushirikiano wa serikali ya Tanzania na Umoja wa Ulaya EU umeendelea kuwa mzuri na akasema EU inaheshimu uhuru wa Tanzania na inaipongeza Tanzania kwa kuweka asilimia 47 ya eneo la nchi yake kwenye hifadhi” Mobhare Matinyi Msemaji Mkuu wa Serikali