Top Stories

Serikali yatoa tamko kwa Nabii aliedaiwa kugundua dawa ya corona

on

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile, amesema kuwa Serikali imekwishatuma wataalam wake kwa ajili ya kumhoji Nabii namba saba aliyejitokeza na kutangaza kuwa anao uwezo wa kutibu ugonjwa wa homa kali ya mafua inayosababishwa na Virusi vya Corona na iliyopewa jina la COVID-19.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa endapo watabaini mtu huyo hana utaalamu katika kile alichokitangaza, Serikali itamchukulia hatua stahiki na kuwataka wananchi kuepuka kutoa kauli ambazo zitachanganya jamii.

“Sisi tumeona hizo clip ambazo zinazunguka na sisi tumetuma timu yetu ya wataalam ili huyo bwana akatuthibitishie kama ana uwezo wa kufanya tiba hiyo na atuambie hiyo dawa yake imesajiliwa wapi na yeye amesajiliwa wapi na lini” Dkt Ndugulile

TANGA UKIINGIA VALENTINE’S KUTOKA MAJAALIWA, JE SAHIHI MWANAUME KUPEWA ZAWADI?

 

Soma na hizi

Tupia Comments