Serikali imewataka wafanyabiashara wa samaki katika masoko ya Jiji la Dar es Salaam kuendelea na biashara zao kama ilivyo kawaida wakati uchunguzi ukiendelea kufanyika kufuatia vifo vya samaki walionekana kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan jana Jumatano Julai 21, 2021.
Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini inasema baada ya tukio hilo, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), maofisa uvuvi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa na meneja wa soko la Magogoni Feri walikusanya samaki kiasi cha Kilogramu 164 na kufikisha Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.