Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichwale amewatoa hofu Watanzania juu ya taarifa za uwepo wa ugonjwa wa homa ya nyani katika maeneo mbalimbali duniani ambapo amesema hadi sasa hakuna mgonjwa wa homa hiyo hapa nchini.
Akizungumza na Wataalamu wa Afya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara Dkt Sichwale amesema kumekuwa na maswali mengi yanayoonyesha hofu kwa Wananchi kuhusu ugonjwa huo,ambapo amesema Serijali inafuatulia kwa ukaribu taarifa za kila Mgeni anayeingia nchini ambapo hadi sasa hakuna Mgonjwa wa homa hiyo hapa nchini.
Amesema Serikali inandelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo ufuatiliaji wa Wasafiri wanaoingia nchini kupitia vituo vyote vya mpakani na tayari Watumishi wamepatiwa mafunzo ya utambuzi wa ugonjwa huo.
Ugonjwa wa homa ya Nyani husababishwa na nyani na panya ambapo Mgonjwa huwa na mwonekano wa malengelenge hasa maeneo ya mkono yanayofanana na ugonjwa wa Tetekuwanga.