Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: ‘Serikali kuanzisha ofisi maalum ya mradi wa LNG, mazungumzo kukamilika Disemba’- Waziri Makamba
Share
Notification Show More
Latest News
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo March 27, 2023
March 27, 2023
Picha: Kutoka kwenye Usiku wa Malkia wa nguvu Mlimani City Hall DSM
March 26, 2023
Hhayuma afunguka uwepo wa Baraza la ardhi Hanang, ‘Nilitaka kushika Shilingi ya Waziri Bungeni’
March 26, 2023
Picha: Mfugaji akamilisha Mjengo wake, aishukuru Kampuni ya Asas kwa kufanikisha ndoto zake
March 26, 2023
Waziri Jafo acharuka, atoa maagizo Mbweni “Wachimba Mchanga, kamata gari, hatua zichukuliwe”
March 26, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > ‘Serikali kuanzisha ofisi maalum ya mradi wa LNG, mazungumzo kukamilika Disemba’- Waziri Makamba
Top Stories

‘Serikali kuanzisha ofisi maalum ya mradi wa LNG, mazungumzo kukamilika Disemba’- Waziri Makamba

September 7, 2022
Share
2 Min Read
SHARE

Waziri wa Nishati, January Makamba, ametembelea ofisi za Kampuni ya Shell, nchini Uholanzi, na kukutana na kuzungumza na viongozi wakuu wa kampuni hiyo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa mradi wa LNG nchini.

Katika mazungumzo hayo na Bwana Cederic Cremers, Makamu wa Rais anayeshughulikia miradi ya LNG na Bwana John Crocker, Makamu Rais wa Shell anayehusika na Mahusiano ya Serikali, Waziri Makamba alielezea azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mazungumzo yanakamilika mwezi Disemba mwaka huu na hatua za utekelezaji zinaanza mara baada ya hapo.

Katika mikutano hiyo, Waziri Makamba pia alielezea mpango wa Serikali wa kuanzisha Ofisi Maalum ya Kusimamia Utekelezaji wa Mradi wa LNG (Tanzania LNG Office) mnamo mwezi Novemba mwaka huu kwa lengo la kuratibu, kuharakisha na kurahisisha hatua za utekelezaji wa mradi.

Mradi huo wa kuchakata na kusindika gesi asilia iliyogundulika katika bahari kuu Kusini mwa Tanzania, utaleta nchini uwekezaji wenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 40, unatekelezwa na Makampuni ya Shell ya Uholanzi na Equinor ya Norway na washirika wao.

Waziri Makamba alieleza kwamba mradi huo una manufaa mengi kwa Tanzania na utafungua fursa nyingi kwa wananchi wa Mikoa ya Kusini mwa Tanzania na kuiongezea mapato nchi na kuleta ajira na mapinduzi ya kiuchumi na kijamii nchini.

Kwa upande wa Kampuni ya Shell, Bw. Crocker, aliishukuru Serikali ya Awamu ya 6, inayoongwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa wawekezaji matumaini na kutoa kipaumbele katika mradi huo na kuwezesha kusainiwa kwa mkataba wa awali. Pia alieleza kuridhishwa kwao kwa hatua ya majadiliano iliyofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo. Bw. Crocker alisisitiza nia yao na ya washirika wao ya kutekeleza mradi.

You Might Also Like

Picha: Kutoka kwenye Usiku wa Malkia wa nguvu Mlimani City Hall DSM

Hhayuma afunguka uwepo wa Baraza la ardhi Hanang, ‘Nilitaka kushika Shilingi ya Waziri Bungeni’

Picha: Mfugaji akamilisha Mjengo wake, aishukuru Kampuni ya Asas kwa kufanikisha ndoto zake

Waziri Jafo acharuka, atoa maagizo Mbweni “Wachimba Mchanga, kamata gari, hatua zichukuliwe”

Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza limefanya misa Takaridu ya Kumuombea Hayati JPM

Edwin TZA September 7, 2022
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article MO Dewji kumpandisha ulingoni Ibra Classic dhidi ya Mmexico
Next Article Jaji aamuru Giggs ashtakiwe upya
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo March 27, 2023
Magazeti March 27, 2023
Picha: Kutoka kwenye Usiku wa Malkia wa nguvu Mlimani City Hall DSM
Top Stories March 26, 2023
Hhayuma afunguka uwepo wa Baraza la ardhi Hanang, ‘Nilitaka kushika Shilingi ya Waziri Bungeni’
Top Stories March 26, 2023
Picha: Mfugaji akamilisha Mjengo wake, aishukuru Kampuni ya Asas kwa kufanikisha ndoto zake
Top Stories March 26, 2023

You Might also Like

Top Stories

Picha: Kutoka kwenye Usiku wa Malkia wa nguvu Mlimani City Hall DSM

March 26, 2023
Top Stories

Hhayuma afunguka uwepo wa Baraza la ardhi Hanang, ‘Nilitaka kushika Shilingi ya Waziri Bungeni’

March 26, 2023
Top Stories

Waziri Jafo acharuka, atoa maagizo Mbweni “Wachimba Mchanga, kamata gari, hatua zichukuliwe”

March 26, 2023
Top Stories

Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza limefanya misa Takaridu ya Kumuombea Hayati JPM

March 26, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?