Michezo

Staa wa soka Uingereza ahukumiwa miaka 6 jela kwa kujihusisha kimapenzi na mtoto

on

March 24 2016 headlines za habari za kusikitisha katika ulimwengu wa soka zimezidi kutawala, ikiwa umepita muda mchache tu toka utangazwe msiba wa nguli wa soka wa Uholanzi na FC Barcelona Johan Cruff, ila zimetoka taarifa za staa wa soka kufungwa jela.

March 24 winga wa zamani wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Uingereza Adam Johnson amehukumiwa miaka sita kwenda jela baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha kimapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 15.

BRADFORD, ENGLAND - MARCH 02: Footballer Adam Johnson leaves Bradford Crown Court on day fourteen of the trial where he was found guilty of one count of child sexual assault charges on March 2, 2016 in Bradford, England. The former Sunderland FC midfielder, 28, from Castle Eden, County Durham, had already admitted one charge of sexual activity with a child and one charge of child grooming. (Photo by Nigel Roddis/Getty Images)

Adam Johnson akitoka mahakamani

Adam Johnson hadi anahukumiwa kifungo hicho alikuwa anaitumikia klabu ya Sunderland ya Uingereza, ambayo toka mwaka 2012 alijiunga nayo hadi 2016, ameichezea jumla ya mechi 122 na kuifungia magoli 19.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andikaAYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments