Leo January 29, 2018 umesambaa ujumbe kwenye mitandao ya kijamii ambao umeandikwa na mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Fredrick Lowassa.
Kwenye ujumbe huo Fredrick ameeleza kusikitishwa na kile alichosema ni taarifa ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr Hamisi Kigwangalla akitaja jina la Lowassa kama mmoja ya watu eti walioshiriki kupora ardhi Arusha.
Ameeleza kuwa akiwa kama msemaji wa familia anazo katika kiganja cha mikono yake taarifa zote za umiliki wowote unaomgusa baba yake Mzee Lowassa.
“Ninaweza kuuhakikishia umma kwamba yote aliyosema Waziri Kigwangalla hayapo na kama anayo basi sisi tuko tayari afanye lolote lililo chini ya mamlaka yake badala ya kurejea kule tulikopita ambako yeye na wenzake kadhaa walifanya bila mafanikio kuchafua heshima za wote anaowataja bila sababu.” – Fredrick Lowassa
BREAKING: Meya DSM ajibu kuhusu dereva wake kudaiwa kutaka kufanya fujo ofisi za CCM