Stori Kubwa

Hii ishu ya watoto kusafiri kwenye chasis ya basi ni moja ya stori kubwa leo May 11 2015

on

Singida KIds

Moja ya story kubwa kuripotiwa na kituo cha ITV jioni hii ni ishu ya watoto watatu wa kiume kukutwa wakiwa wamejificha kwenye chasis ya basi.

Watoto hao wamekutwa Singida ambapo tayari walikuwa wamesafiri kutoka Kahama na walikuwa wakielekea Arusha.

Watoto hao wamesema walitolewa na mtu mmoja Arusha kwenda Kahama akawaambia kuna kazi, walipofika Kahama akawatelekeza, baadae wakaamua kurudi kwa njia hiyo ya kujificha kwenye chasis ya basi.

Kamanda wa Polisi Singida ACP Thobias Sedoyeka amesema watoto hao walikutwa wakati wakaguzi wa mabasi walipokuwa wakikagua basi hilo la Mgamba Express ambapo mpaka wanafika hapo basi lilikuwa limesafiri kwa zaidi ya Kilometa 360.

Habari yote iko hapa kwenye sauti niliyokurekodia..

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyezahapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments