Michezo

Adhabu alizopewa Juma Nyoso na TFF

on

Leo February 13, 2018 Shirikisho la soka nchini TFF kupitia Kamati yake ya  Nidhamu wametoa adhabu kwa Mchezaji wa Kagera Suga Juma Nyoso kutokana na kitendo cha kumpiga shabiki wa klabu ya Simba ambapo Nyoso amefungiwa kucheza mechi tano.

Kamati ya TFF ilikutana February 10, 2018 pia imempiga faini ya Milioni moja mchezaji huyo, ambapo kikao hicho kimejiridhisha kuwa Nyoso alimpiga shabiki huyo.

Nyoso alimpiga shabiki baada ya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya timu yake ya Kagera Sugar dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

MAGOLI YA SIMBA WALIVYORUDI KIMATAIFA LEO VC GENDERMARIE FULL TIME 4-0

 

Soma na hizi

Tupia Comments