Mix

Msg ya kwanza ya Shamsa Ford kwa Mumewe toka aende Polisi kwa sakata la dawa za kulevya

on

Mwigizaji Shamsa Ford ambaye ni mke wa Mfanyabiashara Chidi Mapenzi aliyeitwa Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, ameandika yafuatayo ikiwa ni mara ya kwanza toka aitwe Polisi kuhojiwa.

Shamsa amepost ujumbe huu kupitia Instagram “nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi”

Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya.Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati

Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo ulivyo sasa..Nina amini Mungu anapotaka kukupeleka sehemu anayoitaka yeye lazima akupitishe kwenye mitihani”

Hii ni mitihani ya Mwenyezi Mungu na nina imani inshaallah yatapita..Nakupenda sana mume Wangu kipenzi Rashidi..

VIDEO: ‘Tafuteni njia nyingine za kumchafua mke wangu Shamsa Ford’ – Chiddi

EXCLUSIVE: Hatimae Siwema aongelea ya Jela na Nay wa Mitego kuhusu dhamana na mengine, bonyeza play hapa chini

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments