AyoTV

VIDEO: Vituko na show ya Manfongo na Sholomwamba uzinduzi Ndondo Cup 2017 #Waletee

on

Kama ni shabiki wa burudani ya soka la mchangani taarifa ikufikie kuwa Sports Extra Ndondo Cup 2017 imezinduliwa rasmi leo June 17 2017 katika uwanja wa Kinesi Dar es Salaam, mchezo wa ufunguzi ulikuwa kati ya Stim Tosha dhidi ya Makuburi  ambapo game ilimalizika kwa sare tasa (0-0).

Michuano ya Sports Extra Ndondo Cup 2017 inashirikisha timu 32 lakini kabla ya game ya ufunguzi wa michuano hiyo ambayo tumeona mastaa kama Juma Kaseja, Abdi Banda wa Simba na msanii wa Bongofleva Madee wakihudhuria, yalianza na burudani kutoka kwa wakali wa Singeli.

Wasanii wa Singeli Manfongo na Sholomwamba walikuwa miongoni mwa walioburudisha katika uzinduzi wa Ndondo Cup 2017, huku mashabiki wa Stim Tosha na Makuburi wakinogesha uzinduzi huo kwa vituko na aina mbalimbali ya ushangiliaji.

VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera

Soma na hizi

Tupia Comments