Habari za Mastaa

Shaa ametaja list yake ya Top 5 Most Fashionable Celebrities kwa hapa Tanzania.

on

Sarah Kaisi a.k.a Shaa leo Nov 23 anaingia kwenye headlines kutokana na video yake mpya inaitwa Toba ambayo itatoka leo. Mara nyingi Shaa amekua akisifiwa kwamba yeye ni mmoja kati ya watu maarufu wanaopendeza sana kwenye upande wa mavazi.

Sasa hapa anawataja watu maarufu 5 ambao yeye anasema ndio most fashionable celebrities kwa hapa Tanzania. List hii haijapangwa kwa kuzingatia namba.

1)Madam Rita Paulsen

2
Ni mwanamke ambae anajiamini na anavaa kwa umri wake. Unajua ukishajitambua mimi ni mtu wa aina flani na umri flani lazima ujue nguo gani utavaa na kupendeza. Kuna watu wengine wana force kuvaa nguo ambazo zimewapita umri wao. Lakini Madam Rita anazingatia umri wake na bado anapendeza sana.

2)Nancy Sumari

fsdfd
Ni mwanamke mwenye urembo asilia, kwa ufupi naweza kusema yupo very natural. Unaweza kusema yeye ni mtu ambae anaamka asubui hachagui nguo ya kuvaa, labda anavaa nguo yoyote na bado anapendeza. Unajua sisi wanawake tunapata tabu sana kwenye kuchagua mavazi asubui lakini sidhani kama hii inamtokea Nacy Sumari. Kuna kitu classy about Nacy Sumari kwenye kuvaa.

3)Diamond Platnumz

fdsf
Yeye ni mmoja kati ya wanaume wachache sana kwenye entertainment industry waliohamasisha sana wanaume kuvaa suti na kuwa classic japokuwa wasanii wengi tunategemewa kuvaa vitu colorful. Kuna utofauti mkubwa sana kwenye suti za Diamond, suti zake anazivaa nasio kumvaa nadhani unajua utofauti wake ni nini hapo.

4)Vanessa Mdee

ew
Hamna kitu kigumu kama msanii wa kike kujigundua kama mimi ni brand hii inabidi nivae hivi. Kuna tofauti ya jinsi msanii wa gospel na band wanatakiwa kuvaa, sasa Vanessa amejua brand yake ni ipi na anavaa vile very perfect.

5)Salama Jabir

salama
Huyu ana fashion sense flani very unique, anaweza kuvaa viatu flani vimepigwa spray au vichafuchafu flani hivi ki-fashion lakini bado akatokea poa. Pia Salama ana uwezo wa kuvaa vitu flani na akapendeza lakini mtoto wa kike mwingie huwezi kuvivaa kabisa.

Tupia Comments