Kesi ya Unyang’anyi wa kutumia Silaha namba 105/2021 inayomkabili aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, imeendelea katika mahakama ya hakimu Mkazi Arusha ambapo shahidi wa nne kwa upade wa Jamhuri Hajirin Saad (32) mfanyabiashara wa duka jijini Arusha ameieleza mahakama alivyoombwa rushwa ya sh Milioni 70 na mmoja wa mabaunsa wa Sabaya ili aachiliwe kwenye chumba Cha mateso.