Mkuu wa Mkoa Morogoro Fatma Mwassa amemuapisha Shaka Hamdu Shaka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa.
DC Shaka baada ya kula kiapo hicho ameahidi kutoa Ushirikiano kwa Watendaji wa Wilaya hiyo ili kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi wa Kilosa ikiwemo kutatua migogoro ya Wakulima na Wafugaji.