Katibu wa NEC itikadi na uenezi chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka ametembelea maonesho ya wakulima nanenane kanda ya Mashariki yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Manispaa ya Morogoro ambapo amepongeza jitihada zinazofanywa na wizara ya Mifugo na uvuvi katika utoaji elimu kwa Wafugaji na wavuvi.
SHAKA APONGEZA JITIHADA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
Shaka amesema kitendo Cha wizara hiyo kutoa elimu kwa Wafugaji namna ya ufugaji Bora utasaidia kupunguza changamoto ya wakulima na wafugaji kwani Wafugaji watapata elimu ya kufuga kisasa na kupata manufaa zaidi.
Shaka ametoa wito kwa Wafugaji kufika katika Banda la Wizara hiyo ili kujifunza teknolojia Bora ya ufugaji pamoja na kilimo Cha majani ya malisho.
Shaka amesema Serikali ya awamu ya sita inaendelea kusimamia wizara hiyo pamoja na wizara ya kilimo kwani zaidi ya asilimi 85 ya Wananchi wanategemea sekta hizo hivyo lazima jitihada za makusudi zifanywe ili kuboresha kuinua kipato Cha Wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya uendelezaji maeneo ya malisho na rasilimali za vyakula vya mifugo (DGLF) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,, Bw. Rogers Shengoto amesema wizara hiyo imedhamiria kuinua kipato Cha Wafugaji.
Amesema wizara ya mifugo na uvuvi kwenye maonesho ya Nanenane, imeweza kuonesha teknolojia na maarifa mbalimbali kwa wafugaji, ikiwemo
teknolojia ya uzalishaji wa mbegu za malisho zinazostahimili Teknolojia mbalimbali nchini.
Aidha ameeema Uzalishaji wa vifaranga bora vya samaki pamoja na Uzalishaji wa zao la mwani na uongezaji thamani wa mwani kwa kuzalishaji bidhaa mbalimbali.