Mwimbaji staa kutoka nchini Colombia, Shakira (46) amepigwa faini ya pauni milioni 6.4 ikiwa ni sehemu ya makubaliano yatakayomfanya aepukane na kifungo cha jela na kuhitimisha kesi ya ulaghai iliyoendelea kwa muda mrefu jijini Barcelona nchini Hispania.
Mwimbaji huyo mwenye utajiri unaofikia thamani ya takriban pauni milioni 240, atatozwa faini ya pauni milioni 6.4 (Tsh Bil 19.9) kwa makosa sita ya ukwepaji wa kodi aliyokiri kama ni sehemu ya mkataba uliotangazwa mahakamani leo.
Staa huyo tayari alikuwa amelipa ushuru ambao maafisa wa Hispania walikuwa wamemshtumu kwa kukwepa, ambayo kwa riba kubwa ilifikia karibu pauni milioni 15 Pia atalazimika kulipa faini ya £378,000 (Tsh Bil 1.1) ili kuepuka kifungo cha miaka mitatu jela.
Nyota huyo wa kimataifa alifika katika mahakama ya Barcelona mapema hii leo kwaajili ya kuskiliza kesi yake ya madai ya kulaghai serikali ya Hispania pauni milioni 12.5 (€14.5m) kutokana na mapato aliyotengeneza kati ya mwaka 2012 na 2014.
Suluhu ilifikiwa muda mfupi baadae, huku Shakira ambae jina lake kamili ni Shakira Isabel Mebarak Ripoll akimwambia hakimu msimamizi kwamba amekubali makubaliano yaliyofikiwa na waendesha mashtaka.
Katika taarifa iliyotolewa na timu yake, Shakira alisisitiza kuwa hakuwa na hatia lakini alisema alichukua uamuzi wa kulipa kiasi hicho cha fedha kwasababu asingependa kuwaona watoto kumwona akipitia chanagamoto.