Michezo

Shakira ni mjamzito tena? Hiki alichokisema Gerard Pique

on

10489743_10152593312094596_2669401762394977952_nKwa mara nyingine tena familia ya mwanamuziki maarufu duniani Shakira na mchumba wake mwanasoka, Gerard Pique  – imeingia kwenye ‘headlines’ za vyombo vya haari ulimwenguni.

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ukiwemo mtandao wa tracetv unaripoti kwamba mchumba wa Shakira, Gerard Pique amekaririwa akisema hitmaker wa ‘Hips Dont Lie’ ni mjamzito kwa mara nyingine tena.

Kulikuwepo na tetesi nyingi hasa baada ya Shakira kutumbuiza kwenye kombe la dunia liloisha hivi karibuni nchini Brazil, lakini kambi ya Shakira ilikanusha uvumi huo.

Lakini jana kupitia channel ya kilatino ya “Fox News” – kituo hicho cha TV kiliripoti kwamba Pique amewathibishia kwamba Shakira ni mjamzito.

Pique na Shakira tayari wana mtoto mmoja wa kiume waliyempa jina la Milan, ambaye alizaliwa mnamo mwaka 2012, miaka miwili baada ya wazazi wake kuanza mahusiano yao wakati wa utengenezwaji wa wimbo wa kombe la dunia 2010.

Tupia Comments