Polisi wa Australia siku ya Jumanne walisema shambulio la kisu dhidi ya askofu wa kanisa la Ashuru na baadhi ya wafuasi huko Sydney ni kitendo cha kigaidi kilichochochewa na watu wanaoshukiwa kuwa na msimamo mkali wa kidini, huku nchi hiyo ikiyumba kutokana na tukio la pili la kudungwa kisu ndani ya siku tatu.
Takriban watu wanne walijeruhiwa katika shambulio hilo, akiwemo Askofu Mar Mari Emmanuel wa Kanisa la Assyrian Christ The Good Shepherd, wakati mwanamume mmoja alipompiga kwa kisu wakati wa ibada iliyotiririshwa moja kwa moja Jumatatu.
Tukio hilo katika kitongoji cha Wakeley, magharibi mwa Sydney, lilizua makabiliano nje ya kanisa kati ya polisi na umati wenye hasira wa wafuasi wa askofu huyo ambao walitaka mshambuliaji huyo akabidhiwe kwao.
Polisi walimkamata kijana wa kiume katika eneo la tukio na kulazimika kumshikilia kanisani kwa usalama wake.
“Tunaamini kuna mambo ambayo yameridhika katika suala la itikadi kali za kidini,” Kamishna wa Polisi wa jimbo la New South Wales Karen Webb alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“Baada ya kuzingatia nyenzo zote, nilitangaza kwamba lilikuwa tukio la kigaidi.”
Lakini Webb alisema polisi katika hatua hii ya awali ya uchunguzi wanaamini kuwa mshambuliaji alikuwa anafanya kazi peke yake
Kanisa la Christ the Good Shepherd katika taarifa limetaja shambulio hilo kuwa tukio la pekee na lilisema linasubiri matokeo ya polisi kuhusu nia ya mshambuliaji huyo.
“Kanisa linashutumu kulipiza kisasi kwa aina yoyote,” ilisema