Wasanii wa filamu Jimmy Mafufu na Shamsa Ford wametangaza kujiunga na chama cha Mapinduzi wakitokea CHADEMA wakisema kuwa uwamuzi huo umekuja baada ya kuona maendeleo hanayofanywa na chama cha Mapinduzi kupitia Mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu
Mafufu na Shamsa ambao waliambatana na waigizaji wengine kama JB, Single Mtambalike, Aunt Ezekiel, Kingwendu, Muhogo mchungu na wasanii wa TMK, Juma Nature na Temba bila kumsahau Stamina aliyefunguka kuhusu yeye kuwa mwana chama wa CCM kwa muda mrefu tofauti na ambavyo msanii mwenzake wanaye unda naye kundi moja la ROSTAM, Roma kuwa Chadema
“Mimi ni Mimi na Roma ni Roma, tunatofautiana mitazamo, Ndiomana yeye mrefu mimi mfupi, yeye simba mimi yanga” Stamina