Hatimaye mwanamuziki machachari kutoka nchini Ghana, Charles Nii Armah maarufu Shatta Wale, amekubali ombi la pambano la masumbwi na msanii Burna Boy ili kumaliza chuki kati yao
Wale ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kuandika ujumbe wa kukubali kuingia ulingoni na Burna boy ikiwa ni pamoja na kupendekeza uwanja wa taifa wa michezo wa nchini Ghana, Accra Stadium ndio utumike kukamilisha pambano hilo.
“Oh Burna boy anataka kuzichapa na mimi moja kwa moja, sawa tuifanyie kwenye uwanja huu wa michezo wa Accra. Ikiwa wewe ni mwanaume,” Aliandika.
Licha ya kukubali pambano hilo Shatta Wale bado ameendelea kumshambulia Burna boy kwa maneno makali ikiwa ni pamoja na kukumbushia mambo kadhaa aliyowahi kuyashuhudia kutoka kwa Burna kipindi walichokuwa na mahusiano mazuri.