Habari za Mastaa

Shilole ameizungumzia collabo yake na Iyo wa Nigeria

on

Mwanamuziki staa wa kike ambaye pia ni mjasiriamali Shilole amezungumzia kuhusu Collabo yake na mmwanamuziki wa kike kutoka Nageria Iyo ambaye amewahi kufanya kazi na mkali mwingine kutoka Bongoflevan Diamond Platnumz.

Akizungumza kwenye Sizi kitaa ya Clouds TV, Shilole ameelezea namna alivyohisi baada ya kusikia atafanya kazi na staa kutoka Nigeria akihofia lugha, lakini meneja wa Wizkid ambaye pia ni meneja wa Iyo ameonesha kumkubali na kuzipenda kazi zake kitu ambacho kilikuwa rahisi kwa wawili hao kukutana na kupanga namna ya kufanya kazi.

>>>”Kwanza mimi siyo mtu wa mchezo mchezo. Watu walihisi nitashindwa kuongea naye lugha, lakini tulienda vizuri. Alikuja na Meneja wake ofisi kwangu, Shishi Food, wakala chakula na kukisifia sana. Nilipoambiwa na Gnex kuwa anataka kufanya kazi na mimi, nilimwambia kizungu na mimi itakuwaje ila alinambia she is fine hana shida.

“Meneja wake ananipenda sana na anaelewa kazi zangu. Aliposikia nina ofisi yangu ya chakula, alisema anataka kuniona na kufanya kikao na mimi hapo ofisini kwangu. Kweli alikuja na chakula alikula na tuliongea Kiingereza kizuri.

“Yeye aliingiza sauti bila mimi kufanya chochote na wimbo ulienda Nigeria, ukatengenezwa upya hata beat ipo tofauti na uwimbaji upo tofauti. Base iliyopo ndani ni ya hatari yaani ‘hatutoi kiki Remix‘ ni shida. Siongei kwa sababu ni wimbo wangu ila ni wimbo mzuri.” – Shilole.

Katika hatua nyingine Shilole ametoa ushauri kwa wasanii wengine wa kike ambao wanachipukia kwenye muziki akisema wanatakiwa kuwa na focus na mwenendo mzuri>>>”Kuna wasanii wengine wanasema wanataka kuwa kama Shishi, lakini hawana focus. Kama hauna focus huwezi kwenda mahali, utaishia kuwa underground sugu kwa kuwa hauna muongozo. Kwa hiyo, niwasihi tu, wanatakiwa kuweka nguvu kwenye muziki maana muziki kama unaupenda utakupenda pia.” – Shilole.

VIDEO: Dulla Makabila kwenye stage ya Wasafi.com Mbagala

Soma na hizi

Tupia Comments