AyoTV

VIDEO: Rais Shein aweka wazi mazungumzo waliowahi kuyafanya na Maalim Seif

on

January 11 2017 kupitia kipindi cha Funguka cha Azam TV, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amezungumzia kwa mara ya kwanza, mazungumzo aliyowahi kuyafanya na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Maalim Seif alijiondoa kwenye mazungumzo hayo ya maridhiano baada ya kufanyika kwa takribani vikao kadhaa, huku wajumbe wake wakiwa pamoja na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Dk. Salmin Amour Juma, Amani Abeid Karume na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.

Akizungumza Rais Shein kwenye mahojiano hayo amesema …….>>>mazungumzo kweli tumefanya yalianza vizuri, yeye hakutaka kurudia uchaguzi, mimi nikasema tume imetangaza sio mimi, nikasema tume ikitangaza kuwa turudie mimi na chama changu tutakubali, lakini yeye akakataa’

VIDEO: Madai yaliyoibuka ndani ya CUF kuhusu wizi wa fedha, Bonyeza play hapa chini 

Soma na hizi

Tupia Comments