Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ameongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya jukwaa la @shuledirect ambao ni wabobezi wa utoaji wa elimu kidigitali kupitia mtaala wa Tanzania kielimu.
DC Mpogolo amewapongeza shuledirect kwa ubunifu na uthubutu katika mchakato wa kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi wa Tanzania akiahidi msaada wa serikali katika chochote ambacho watahitaji kwani wanachokifanya ni kuunga mkono jitihada za Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu bora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule Direct @farajanyalandu ameleza kuhusu mafanikio ya safari ya miaka 10 ya @shuledirect akieleza namna ambavyo walianza kwa watumiaji 0 hadi leo ambapo wanahudumia zaidi Wanafunzi million 4 Duniani kote, mwamko wa Walimu katika matumizi ya jukwaa hili, kuchukua rasilimali za kufundishia na mengineyo mengi.