Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) leo imeingia mkataba wa miaka mitano wa udhamini na Bank ya CRDB pamoja na mbunifu wa mavazi Sheria Ngowi.

Mkataba huo wa miaka mitano utaiwezesha Zanzibar Heroes kupatiwa vifaa vya michezo pamoja na jezi zilizobuniwa na Sheria Ngowi ambaye ndio mbunifu Mkuu wa jezi za Yanga SC.

Mkataba huo umesainiwa Golden Tulip Hotel visiwani Zanzibar ukisainiwa na Rais wa Shirikisho la mpira Zanzibar (ZFF) Abdullarif Ali Yassin, Sheria Ngowi.

Pamoja na Afisa Mkuu wa Biashara CRDB Boma Raballa mbele ya ushuhuda wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita.
