Wabunge wa Gambia walitathmini katika Bunge la taifa Jumatatu Machi 18, 2024 kuondolewa kwa marufuku ya ukektaji nchini.
Hatua hii hatimaye haikupigiwa kura na, kwa mujibu wa taarifa zetu, itaenda kwa kamati kwa ajili ya kupiga kura, ambayo tarehe yake haijatangazwa. Mamia ya watu walikusanyika mjini Banjul kupinga marekebisho ya sheria hiyo. Kwa nini wabunge wa Gambia wanarejea kwenye marufuku hii ya ukeketaji ya mwaka wa 2015?
Mbunge aliyewasilisha mswada huu anatumia hoja za kidini na kimila. Kulingana na mbune huyo na mashirika ya kidini, kupiga marufuku tabia hii kunakiuka haki ya watu wa Gambia kutekeleza utamaduni wao na mila iliyokita mizizi.
Kwa hakika, ukeketaji umeendelea kutekelezwa kwa wingi nchini Gambia, hata tangu kupigwa kwake marufuku: 73% ya wasichana na wanawake wa Gambia wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamekeketwa nchini humo. Wengi wao walikuwa kabla ya umri wa miaka 5 kulingana na takwimu za 2024 kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto.
Mashirika mengi ya kiraia yanazitaka mamlaka kutokubali shinikizo kutoka kwa makundi yenye msimamo mkali.