Habari za Mastaa

Miss TZ Diana amewajibu wanaosema kapewa gari lenye mabango

on

Baada ya Miss Tanzania 2o16 Diana Edward kukabidhiwa zawadi ya gari aliloahidiwa kufuatia ushindi kwenye shindano lililofanyika October 2016, gari hilo limekuwa gumzo mitandaoni kutokana na mabango yaliyowekwa kwenye gari hilo.

Kupitia Leo Tena ya Clouds FM leo May 12, 2017 Miss Tanzania 2016, Diana Edward amesema anatoa shukrani na anawaunga mkono waandaaji na hawezi kuwazuia watu kusema kwa kuwa hawafahamu namna gani wamepambana kulipata gari hilo.

“Mabango yatatolewa siku hizi mbili na nimefundishwa kushukuru. Kwa hiyo, nilichopewa nimeshukuru. Nitaliendesha gari, sina kipingamizi. Maneno, watu watayaongea, hiyo ipo. Hakuna binadamu anayekubali kitu. Ndio uwezo wao ulipofikia wa kunipa hiyo zawadi.

“Siwezi kuwapinga – ninawaunga mkono. Mimi ni binadamu pia, kwa hiyo, nimepewa zawadi na nimepokea kwa shukrani, na nawashukuru Kamati na wadhamini na watu wote walioshiriki mpaka nikapata gari.

“Sijui wanachokiongea, ila hali halisi ndio hiyo. Niliitwa nikaambiwa gari lako ndio hili. Nikalipokea kwa shukrani. Mimi sijali watu wanasema nini, maana maneno yapo. Wao wamenipa walichokiweza kwa sababu wamehangaika kweli kulitafuta hilo gari. Watu hawawezi kujua kwa sababu wapo kwenye social media, lakini wangekuwepo tangu watu wanahangaika kulipata hilo gari tangu mwezi wa 6 mpaka leo hii wmaepata.” – Diana Edward.

Alichosema Miss TZ Diana baada ya kupewa gari lake miezi 6 baada ya fainali (+video)

Soma na hizi

Tupia Comments