Habari za Mastaa

U HEARD: Shilole adaiwa kusababisha hasara ya Tsh. milioni 9.2 kwa Promoter

on

April 18 2017 kupitia U-heard ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brown ametuletea stori hii kuhusu hasara inayodaiwa kusababishwa na Shilole kwa Promoter aliyekuwa ameandaa show siku ya Sikukuu ya Pasaka Visiwani Zanzibar.

Staa huyo anadaiwa kusababisha hasara ya Tsh 9,200,000 ikitajwa sababu kubwa ya hasara hiyo ni kuchelewa kupanda kwenye stage nikuchelewa kuperform ambapo ili kujua undani wa stori hiyo Soudy alizungumza na Promoter huyo pamoja Shilole>>>“Show ilienda ovyo, Shishi alikuja saa saba kasoro usiku, na show ilitakiwa kuanza saa 2 mpaka saa 6 usiku kwa sababu ukumbi wa pale, mwisho ni saa 6. Ni hasara kubwa, lakini atailipa.” – Promoter.

“Huo ni uwongo. Siyo kweli, hakuna show ya saa 2, labda Disco toto. Halafu huo ni uwongo na show zetu zinajulikana ni saa 7 na kuendelea.” – Shilole.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full Story

VIDEO: Show ya Navy Kenzo mjini Tel Aviv Israel

Soma na hizi

Tupia Comments