Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric James Shigongo wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ameomba Wizara kuangalia uwezekano wa kufanyia marekebisho sheria ili impe ulinzi Mkurugenzi wa TAKUKURU kama ilivyo kwa CAG na kumfanya aweze kutimiza majukumu yake bila kuwa na hofu ya kupoteza kazi yake.
“Tukatae tukubali wapo Watu kwa simu moja tu mambo yanaweza ya kabadilika na ushahidi unaweza ukaharibika na kesi isifike Mahakamani, tumpe uhakika Mkurugenzi wa TAKUKURU”