Habari za Mastaa

Shilole amlilia Magufuli kumtumbua alieshindwa kuapa, aomba ateuliwe U-DC (+video)

on

Ni headline kutokea kwa staa wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni Mjasiriamali Zena Mohammed maarufu kama Shilole akifunguka kwenye Exclusive interview na AyoTV ambapo amemuomba Rais Magufuli kama ikimpendeza amteue katika nafasi ya Ukuu wa Wilaya licha kwamba elimu yake ni ndogo lakini anaamini katika uwezo wake wa kuwatumikia wananchi.

Shilole pia ametumia nafasi hiyo kumuomba Rais Magufuli amtafutie nafasi nyingine Francis Ndulane ambaye aliyeuliwa kuwa Naibu Waziri lakini akashindwa kula kiapo mbele yake na kuamua kumtumbua.

Soma na hizi

Tupia Comments