Top Stories

Shirika la Afya lakabiliwa na upungufu wa vifaa Afghanistan

on

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema lina vifaa vya kudumu wiki moja pekee Nchini humo baada ya vifaa vya matibabu kutoka nje kuzuiwa kutokana na vizuizi katika Uwanja wa Ndege wa Kabul.

Pia limeeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya sasa kushinikiza maambukizo ya COVID19. Imeelezwa, upimaji umeshuka kwa 77% katika wiki iliyopita na zoezi la chanjo nalo limedorora.

Maafisa wa WHO wamesema 95% ya vituo vya afya viliendelea kufanya kazi lakini baadhi ya wafanyakazi wa kike hawajarudi kwenye vituo vyao, na wagonjwa Wanawake wanaogopa kutoka nyumbani.

UTACHEKA VITUKO VYA CHOLO, NDUGU WAANDISHI WA HABARI, UKWELI WA MAISHA YAKE, KICHAA, SURA YAKE

Soma na hizi

Tupia Comments