Habari ya Asubuhi na karibu kwenye matangazo yetu hii leo….
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amepokea vifaa vya kisasa vya kilimo vya ndege nyuki (drone) na vishkwambi 370 kutoka Shirika la Chakula Duniani (WFP) leo tarehe 28 Agosti 2023, jijini Dodoma.
Waziri Bashe amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kukabiliana na visumbufu vya mazao shambani ili kilimo kiwe na tija katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema drone hiyo kubwa yenye uwezo wa kupulizia dawa na viuatilifu katika hekta 20 na vishkwambi 370 vyenye thamani ya shilingi milioni 364 vitarahisisha utekelezaji wa dhana ya kilimo ni sayansi kwa kuwa vitatatua changamoto za Wakulima.
“Nawashukuru sana WFP kwa kutupatia vifaa hivi, ambapo vishkwambi vinakwenda kugawiwa kwa Maafisa Ugani kwa ajili ya kukusanya taarifa mbalimbali za Kilimo,” amesema Waziri Bashe.
Mhe. Waziri Bashe ameeleza kuwa vifaa vya drones na vishkwambi 370 vitaanza kutumika kwa kupima mashamba ya vijana wa programu ya Jenga Kesho iliyo Bora