Ad
Ad

AyoTV

VIDEO: Tutofautiane kwa itikadi zetu lakini tuangalie maslai ya wananchi’ –Mbunge Kishoa

on

Mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA Jesca Kishoa alisimama bungeni na kuonesha kutopendezwa na baadhi ya wabunge ambapo wamekuwa wakitoa lugha za kejeli kwa viongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni huku akitaka wabunge kuzingatia maslai ya wananchi kuliko vyama.

Kishoa amesema…>>>‘Leo hii nchi yetu tumekosa fedha za MCC takribani dola 463 kutoka Marekani kwa sababu ya ukosefu wa utawala bora, Waziri wa fedha amezunguka nchi zote za ulaya amekosa mikopo kwa sababu kigezo namba moja cha mkopo ni  lazima kuwe na utawala bora

Hadi leo bajeti ya mwaka 2016/2017 imetekelezeka kwa asilimia 34 tu kwa sababu kubwa ya ukosefu wa utawala bora, wawekezaji na wafanyabiashara wanakimbia kwa sababu hakuna mwekezaji anaweza kuwekeza kwenye nchi ambayo muda wowote mkataba unafunjwa kwenye majukwaa’ – Jesca Kishoa

VIDEO: Halima Mdee Vs Goodluck Mlinga Bungeni 

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments