Baada ya taarifa kusambaa kuwa Mrembo Hamisa Mobeto ambae ni Mzazi mwenzake na Diamond Platnumz kwamba amempeleka Staa huyo Mahakamani kwa madai ya kutomuhudumia mtoto wake, Mwanasheria wa kujitegemea Jebra Kambole amefungua picha kamili ya sheria yenyewe.
Jebra amesema “Kwanza Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inapiga marufuku kwa mtu yeyote ambae ni Mwandishi wa Habar kutoa taarifa au picha za Mtoto ambae kuna kesi yake Mahakamani lakini kwa kesi ambazo zinahusiana na Wazazi au madai ya matunzo ya mtoto hiyo sio kesi ya mtoto bali ya Watu wazima”
“Kesi za Wazazi kwa Wazazi Baba na Mama wanapopelekana kuhusu matunzo ya mtoto ni kesi ambazo ni za kimadai na zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya madai, Wazazi wanapodaiana kuhusu matunzo Mahakama inazingatia kuangalia zaidi mtoto wakati wa kuendesha shauri hilo”
“Mahakama mara nyingi kwenye kesi kama hii inazingatia madai na kuyapima, wakati wa kutoa gharama za matunzo Mahakama inaangalia vitu kadhaa ukiwemo uwezo wa kipato cha Wazazi wote wawili lakini pia inaangalia majukumu ya kiuchumi ya Mzazi anaedaiwa”