Michezo

Rasmi Niyonzima sio Mwekundu, kukutana na Simba Kimataifa

on

Baada ya kuvitumikia vilabu vya Simba na Yanga kwa miaka kadhaa, hatimaye Haruna Niyonzima leo  amerejea nyumbani rasmi nchini Rwanda kwa kukamilisha usajili wa kuwatumikia Mabingwa wa Rwanda Cup, Klabu ya AS Kigali inayoshiriki ligi ya nchi hiyo.

AS Kigali pia inatarajia kushiriki katika michuano ya shirikisho Barani Afrika, Niyonzima ni miongoni mwa wachezaji 8 wapya wa AS Kigali, wakiwemo wanyarwanda wanne – Haruna Niyonzima, Ndayishimiye Eric Bakame, Rusheshangoga Michel, & Ishimwe Christian.

Wengine wanne ni wachezaji wawili kutoka Gabon na wawili kutoka Cameroon.

MAGUFULI ALIVYOSIMAMISHA DALADALA, ABIRIA WAFUNGUKA MIMI NI CHADEMA ILA NIMEFURAHI

Soma na hizi

Tupia Comments