Mix

Shuhuda asimulia Zungu alivyochomewa ndani “alilia naungua” (+video)

on

Mmoja wa Mashuhuda kwenye tukio la Hamisi kudaiwa kuchomewa ndani ya nyumba na girlfriend wake aitwae Neema anaendelea kusimulia kilichotokea baada ya kugundua Hamisi kafungiwa ndani na moto unawaka.

“Nilimwambia fungua mlango akasema siwezi kufungua ikabidi nianze kufanya ustaarabu wa kumtoa mtoto wangu, nikwambia ngoja nitoke nje niombe msaada wa watu kuja kunisaidia maana peke yangu siwezi akanijibu sawa Mama Su fanya haraka”

“Nikaanza kutoka nje kukimbia naomba msaada wa Watu, nimetoka nikazunguka nikazunguka naita Watu kwa usiku ule walikuja baadhi kama watatu tu wakawa wanaangalia jinsi ya kusaidia kuhangaika hangaika hadi kuja kubomoa Zungu akawa haongei tena maana hadi watu wanafika alikuwa anaendelea kulia naungua…naungua…nisaidie majirani naungua”

“Hadi kuja kusukuma mlango tayari Zungu akawa kaacha kuongea, kwenye nyumba tulikuwa tunaishi wawili mimi na yeye(Neema/Grace).

“Baada ya hapo kuna Boda boda walikuwa wanapita tukawa tunaomba msaada watoe taarifa Polisi, Polisi wakaja wakawapigia simu FIRE ambapo wakaja wakazima moto na kufanikiwa kumtoa Zungu na hadi moto unawaka Neema hakuwepo ndani ya nyumba,” amesema Shuhuda (Mama SU).

DIAMOND PLATNUMZ AAGIZA LAMBORGHINI NA BENTLEY, MAGARI YA MABILIONEA

Tupia Comments