Haya ni maelezo ya shuhuda Mohamde Hamis ambae alikua miongoni mwa abiria ndani ya boti.
1. Boti ilipofika Nungwi sehemu yake ya mbele ilizama na mabegi yake na iliporudi juu ikazima na kuzunguka palepale, dakika tano baadae ikawaka ndio tukaondoka watu wengine wakiwa wamebaki kwenye maji wanaelea.
2. Baada ya boti kuwaka ndio wale watu waliobaki kwenye maji wakatupiwa viokozi vya upepo ndio boti ikaendelea na safari.
3. Hatujui ni watu wangapi waliobaki kwenye maji ila hakuna baharia hata mmoja alieshuka kutoka kwenye boti kwenda kwenye maji.
4. Tulipokaribia bandarini Znz tulitangaziwa kwamba hatutapelekwa bandarini kushuka mpaka tuvue life jacket tulizozivaa baada ya dhoruba ili tusionekane nazo manake walitaka habari zisivuje.
5. Wale waliorushwa kwenye maji walichukuliwa na wimbi, watoto na watu wazima nilikua nawaona kabisa wametupwa kwenye maji.
6. Sehemu ya watu walioachwa baharini ni miongoni mwa waliokua wamelala kwenye sehemu ya boti iliyozama, kina mama na wengine waliowepesi kutapika ndio ilibidi wakae nje kwenye hii sehemu ili wapigwe na upepo.
7. Ni ngumu kujua walikua watu wangapi waliokuwemo pale mbele kwenye sehemu iliyozama ila ni zaidi ya 20.
Kwa uthibitisho zaidi unaweza kumsikiliza huyu shuhuda hapa chini..