Shule ya Nuru Angavu iliyoko Mwanagati, Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam imefanya vizuri Matokeo ya Darasa la saba kwamwaka 2023 , Ki-mkoa imeshika nafasi ya nane kwa upande washule zenye idadi ya watahiniwa chini ya 40 kwa darasa.
Meneja wa shule hiyo ya mchepuo wa Kiingereza Mary Kimaroanasema kuwa siri ya mafanikio ya shule yake ni ushirikianobaina ya wazazi waalimu na mamlaka zinazosimamia elimuhapa nchini.
“Bila ushirikiano huo tusaingefikia hapa, utaona umuhimu waushirikiano katika kufanikisha jambo lolote lile,” anasema.
Anatoa wito kwa wazazi kuwa maeneo yanayoizunguka shuleyao na Jijini la Dar es Salaam kwa ujumla kuhakikisha kwambawanawapeleka watoto wao shuleni hapo kama wanataka wapateelimu bora.
Anasema shule yake imeomgoza katika Kata yao ya mzinga nakwamba wamejipanga kufanya vizuri zaidi siku zijazo.
Anasema kwamba wamejipanga kukuza vipaji vya vijana iwekatika masomo au katika michezo kwa ujumla kwani vipajikatika Dunia ya sasa vinalipa sana.
Anasema shule yake pia inasomesha vijana 30 bure ambaowanatoka katika familia duni lakini wakiwa na uwezo wakimasomo.
“Tunasaidia vijana hawa ili kuwawezesha kupata elimu bora hata kama hawana uwezo wa kiuchumi.
Anatoa wito kwa taasisi mbalimbali kushirikiana na taasisi yakekatika kuwasaidia vijana hao.