Ofisi ya Kamishna wa Kulinda Data imeipiga faini taasisi ya elimu kwa kukosa kutii Sheria ya Kulinda Data.
Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, Shule ya Roma yenye makao yake mjini Uthiru, Nairobi, inadaiwa kuchapisha picha za watoto wadogo bila idhini ya wazazi.
Kulingana na kamishna huyo, hii ni adhabu ya kwanza na ya juu zaidi kwa kituo cha elimu kutolewa ikiwemo faini ya $31,000 (£25,000) kwa kuchapisha picha hizo.
Hii ni hatua ya kwanza ya aina yake kuchukuliwa na Ofisi ya Kamishna wa Ulinzi wa Data.
Walibainisha taasisi hizo zitapata somo kutokana na adhabu ya kutotumia takwimu za watoto wadogo bila ridhaa ya wazazi.
“Hii inatuma ujumbe kwa shule na vituo vingine vinavyoshughulikia data za watoto ili kupata ridhaa kutoka kwa wazazi/walezi kabla ya kuchakata data za watoto,” inasomeka taarifa hiyo.