Washirika wa Mnazi Bay (Wentworth Gas Limited, M&P Tanzania na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wamekabidhi maktaba mbili kwa shule za sekondari Naliendele na Mahurunga zilizoko mkoani Mtwara. Hii ni sehemu ya ushirikiano wa mpango wa shirika kurudisha kwa jamii (CSR). Washirika wa Mnazi Bay (Mnazi Bay Partners) inashiriki makubaliano ya rasilimali katika Mnazi Bay.
Mradi wa maktaba, ni matokeo ya ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali, katika mkakati wa READ (Realising Education for Development) kama washirika wa utekelezaji, Mradi huu umezipatia shule za Naliendele na Mahurunga vitabu 2030, computer 6 na samani za ofisi. Zaidi ya walimu 30 wamepata mafunzo kuhusu usimamizi wa maktaba na matumizi ya mbinu za kisasa za kufundishia na takribaki wanafunzi 920 wamepokea mwingozo kuhusu namna ya kujisomea kwaajili ya kuwahamasisha na kukuza tabia ya kusoma.
Mgeni rasmi katika hafla ya makabidhiano hayo alikuwa Mohamed Longoi ambaye aliyemwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara. Mtwara Regional Administrative Secretary (RAS). Maofisa wengine wa serikali ambao walihudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Adam Shaningo, Afisa Elimu ya Msingi wa Wilaya Adam Shaningo
“Programu ya shirika kuwajibika kwa jamii (CSR) ya Wentworth imetoa fedha za ufadhili kwa ajili ya: (i) Mfumo wa kuvuna maji ya mvua uliojengwa katika mji wa Kitangali wilayani Newala; (ii) Imesaidia kazi ya upanuzi wa jengo la makumbusho la Mikindani kupitia TradeAid; (iii) Imesaidia mradi wa Hosptali ya Taifa ya Muhimbili wa kuongeza ufahamu kuhusu seli mundu, mradi ambao ulifanyika katika shule 6 za sekondari mkoani Mtwara kikiwemo Chuo cha Afya na Sayansi shirikishi cha Mtwara pamoja na Hospitali ya rufaa ya Ligula” Richard Tainton, Meneja Mkazi wa Wentworth Gas Limited Nchini
Jumla ya wanafunzi 2500 na walimu walikutana na timu ya wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (iv) Walisaidia mradi wa Hospitali ya CCBRT wa kuongeza ufahamu kuhusu tatizo la Festula na Mdomo wazi. Timu ya wataalamu kutoka Hospitali ya CCBRT walitembelea wilaya 6 za mkoa wa Mtwara na zaidi ya watu 3,000 waliweza kufikiwa kupitia matangazo ya redio na kupitia kutembelea katika vituo vya afya na maeneo ya umma” Richard Tainton, Meneja Mkazi wa Wentworth Gas Limited Nchini
Jumla ya wanawake 5 na watoto 2 waliweza kufika katika Hospitali ya CCBRT kama matokeo ya mpango huu wa wiki mbili wa kuongeza ufahamu (v) Pia tulitoa msaada katika wodi ya watoto wenye ugonjwa wa kansa katika hospitali ya Muhimbili. Ambapo michango ilifanyika ikiwemo ya kusaidia ununuzi wa dawa za kansa na kuwapatia mfanzo wataalamu 4″ Richard Tainton, Meneja Mkazi wa Wentworth Gas Limited Nchini
“Kupitia ushirikiano wetu na serikali ya mkoa wa Mtwara, Kampuni ya M&P imejitolea kusaidia jamii kiuchumi, kijamii na kimazingira. M&P imeweza kusaidia miradi mingi ya kuwajibika kwa jamii (CSR) katika miaka 10 ambayo imeendesha uchimbaji wa gesi nchini Tanzania Miradi hiyo” Nicolas Engel Mkurugenzi Mtendaji wa M&P Tanzania
“Jitihada za kuboresha elimu kama vile ujenzi wa vyumba vya madarasa, majengo ya utawala ya shule na nyumba za walimu; (ii)Jitihada za kuboresha huduma kwa mama wajawazito kama vile kujenga wodi ya wajawazito katika hospitali ya kijiji cha Msimbati; (iii) miradi ya afya kama vile ujenzi wa vyoo na visima vya kuchimba, (iv) Miradi ya mazingira kama vile usafi wa mazingira (Siku ya usafi duniani) na miradi mingine mingi katika Mkoa wa Mtwara”. Nicolas Engel Mkurugenzi Mtendaji wa M&P Tanzania