Magazeti

Umeisikia hii ya mkaa,mihogo mikavu kutumika kama chaki ubaoni huko Kagera?

on

tichaa

Ukiisoma habari hii inaweza kukuchekesha lakini ina ukweli ndani yake na wala si masihara hata kidogo baada ya walimu waliojitolea wa Shule ya Msingi Msali Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera kutumia vipande vya mihogo mikavu na mkaa kuandika ubaoni baada ya kukosa chaki.

Hata mimi imenishangaza kidogo kusikia mkaa unatumika kwenye ubao mweusi lakini Mwandishi wa habari hii kutoka Gazeti la MWANANCHI alithibitisha hilo na kusema wamekua wakipata shida sana kufundisha kwa vitendo hivyo kulazimika kutumia mihogo na mikaa ili kufikisha elimu kwa wanafunzi wao.

Wakizungumza shuleni hapo walimu hao ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema hawana chaki za kuandikia na kwamba wanatumia vitabu viwili vya hesabu na kiswahili kufundishia wanafunzi zaidi ya 200.

dent

Mwalimu mkuu wa Shule hiyo Evaline Jeremiah alisema shule hiyo ilianza mwaka jana kutokana na uwapo wa watoto wengi ambao hawajaenda shule lakini haijasajiliwa.

Alisema wazazi walianzisha banda la kuwafundisha watoto kusoma,kuandika na kuhesabu hivyo kusaidia kuajiri vijana waliomaliza kidato cha nne.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

 

Tupia Comments